1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Heiligendamm: Russia yasubiri jawabu kuhusu kituo cha kukinga makombora.

9 Juni 2007
https://p.dw.com/p/CBtT

Russia imesema inatarajia jawabu la kuridhisha kutokana na pendekezo ililolitoa la kushirikiana kujenga kituo cha kukinga makombora barani Ulaya.

Afisa mmoja mkuu wa Russia amesema Rais George W. Bush amevutiwa na mapendekezo ya Russia kwamba Marekani ijenge kituo hicho nchini Azerbaijan.

Rais wa Russia, Vladmir Putin, alitoa mapendekezo hayo siku ya Alhamisi iliyopita baada ya kupinga vikali mpango wa Marekani wa kujenga kituo hicho nchini Poland na Jamhuri ya Czek.