1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Hezbollah wadai kudungua droni ya Israel karibu na Lebanon

26 Juni 2023

Kundi la wanamgambo wa Hezbollah nchini Lebanon, limesema wapiganaji wake wamedungua ndege isiyoendeshwa na rubani ya Israel iliyokuwa ikiruka kwenye anga la karibu na mpaka kwenye eneo la Kusini mwa Lebanon

https://p.dw.com/p/4T4se
Israel | Drohne der Hisbollah
Picha: IDF/AFP

Kundi la wanamgambo wa Hezbollah nchini Lebanon, limesema wapiganaji wake wamedungua ndege isiyoendeshwa na rubani ya Israel iliyokuwa ikiruka kwenye anga la karibu na mpaka  kwenye eneo la Kusini mwa Lebanon.

Hata hivyo kundi hilo halikutowa maelezo zaidi kuhusu aina ya droni iliyodai kuidunguwa karibu na kijiji cha Zibqine kaskazini mwa mpaka kati ya Lebanon na Israel.

Kadhalika Israel haikutowa tamko la haraka. Tukio hilo limekuwa baada ya wiki kadhaa za kuwepo mivutano kwenye eneo la mpaka baina ya nchi hizo mbili na hasa katika eneo lenye mvutano linalojulikana kama mashamba ya Chebaa.