1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Hoteli iliyoshambuliwa na Al Shabaab yadhibitiwa Somalia

Saumu Mwasimba
29 Novemba 2022

Vikosi vya usalama nchini Somalia vilifanikiwa jana Jumatatu kumaliza mzingiro wa kundi la Alshabab katika hoteli moja waliyokuwa wameiteka katika mji mkuu Mogadishu.

https://p.dw.com/p/4KERh
Somalia Mogadishu | Al-Shabaab Kämpfer während Militärübung
Picha: Farah Abdi Warsameh/AP/picture alliance

Katika tukio hilo watu tisa waliuwawa kwenye jengo lililotekwa na Alshabaab karibu na makaazi ya rais,kwa mujibu wa polisi.

Milio ya risasi ilisikika kutoka nje ya hoteli hiyo wakati vikosi maalum vya usalama vilipokuwa vikipambana na wanamgambo hao zaidi ya saa 12 baada ya kuvamiwa hoteli hiyo. 

Tukio hilo la hujuma limeonesha uwezo wanaoendelea kuwa nao Alshabab ambalo ni kundi linalofungamanishwa na mtandao wa kigaidi wa al Qaeda,wa kufanya mashambulizi yanayoweza kusababisha wakati mwingine mauaji ya watu wengi katika mji huo mkuu wa Somalia.

Hujuma za kundi hilo zimefanywa katika wakati ambapo serikali ya  rais Hassan Sheikh Mohamud  inaendelea na operesheni ya kijeshi dhidi ya kundi hilo.

Chanzo: reuters