1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Hotuba ya Rais Kohler imepokewa vipi Ujerumani ?

25 Machi 2009

Rais Kohler ahutubia jana Taifa.

https://p.dw.com/p/HJIJ
Horst KöhlerPicha: picture-alliance/ dpa

Maoni ya wahariri wa magazeti ya leo ya Ujerumani yametuwama mno juu ya hotuba ya jana ya Rais Horst Kohler wa Ujerumani kwa Taifa ikigusia msukosuko wa fedha wa hivi sasa.Hata mkutano wa jana wa Rais Barack Obama wa Marekani na waandishi habari juu ya vipi kuuimarisha uchumi wa Marekani kukabiliana na msukosuko huo wa fedha imechambuliwa. Ramadhan Ali akiwakagulia safu za wahariri leo, anaanza na

Gazeti la LAUSITZER RUNDSCHAU kuhusu Obama. Laandika:

"Kile ambacho Rais Barack Obama wa Marekani alichopitisha punde ili kuyaokoa mabenki ya nchi yake na kuona yanafanya kazi ni sawa na kuuzima moto kwa njia ya kuuzuwia tu usitapake: Kwa kufanya hivyo,Obama pia anajitwika hatari kubwa za kisiasa mabegani mwake .Kwani kwa baadhi ya watu itakuwa vigumu sana kuridhia kuwa majambazi wale wale waliosababisha kuporomoka kwa masoko ya fedha na mabenki sasa wanapewa uwezo wa kuuza upya mahikalu waliosababisha na kuvuna tena fedha.

Iwapo wananchi wa Marekani watameza kidonge hiki kichungu,itategemea zaidi kwsa haraka gani mafanikio ya hatua hii yatachomoza."

Gazeti la LANDESZEITUNG kutoka Luneburg linaichambua hotuba kwa taifa aliotoa jana Rais Horst Kohler wa Ujerumani : Laandika:

""Dola imara zaidi,uadilifu zaidi,haki zaidi na dhamana zaidi-hizo ndizo nguzo za kimsingi za mapinduzi ya kiviwanda na kimazingira ambayo Rais Kohler alizungumzia katika hotuba yake ya Berlin hapo jana.Mtaalamu huyu wa uchumi ameukosoa mfumo wa fedha ambao binafsi anatokana nao alipokuwa mkurugenzi wa wa Shirika la Fedha Ulimwenguni (IMF).

Katika jamii ambayo kwa muda mrefu ikiishi kupindukia pato lake , kujikosoa huko sio tu hotuba ya Rais Kohler imepokewa vyema na wananchi,bali mseto aliowasongea wa mchanganyiko wa pongezi na kuwakaripiwa ,kuwashajiisha na kuwaonya ameusonga vizuri .Hatahivyo, kwa wanasiasa wengi na mameneja wa mabanki,viungo alivyowatilia havikuwa vikali kuwazuwia kurejea tabia zao za zamani."

Ama gazeti la Schwabische Zeitung likiichambua nayo hotuba ya Rais Kohler wa laandika:

"Katika ile hotuba muhimu kabisa ya awamu yake , Rais Kohler amepigiwa makofi na kushangiriwa na kambi mbali mbali.Matarajio yalioegemezwa juu ya hotuba yake kabla kuitoa, yalikuwa makubwa,tena kwa sababu mbili:

Kwanza, Kohler ,ni mwanabanki wa kwanza kuwa Rais wa Ujerumani ambae kauli yake wakati wa msukosuko wa sasa wa fedha ,ina uzito.Pili, ni rais wa kwanza wa Ujerumani anaegombea wadhifa huo atakaekuwa na mpinzani. Na Rais Kohler amezikabili changamoto hizo mbili barabara. Ameonesha mkondo wa kufuatwa, hakuficha matatizo yaliopo,ametaja nguzo za kiadilifu na kushajiisha njia ya kunyosha.Inahitajika kuwa na akina Kolher wengi zaidi kama yeye serikalini."

Gazeti la "DER NEUE TAG" latukamilishia kwa kuandika machache tu:

"Misukosuko daima hutoa pia nafasi ya kurekebisha mambo.Rais Kohler ni mfano halisi.Imesadifu miezi 2 tu kabla ya uchaguzi mpya wa rais wa Ujerumani ,ametoa hotuba ambayo hata wale wenye shaka shaka nae imewatuliza."

Mwandishi: Ramadhan Ali

Mhariri: Mohammed Abdulrahman