1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Merkel lazima amshinikize Putin kuhusu haki za binadamu

Yusra Buwayhid
17 Agosti 2018

Shirika la Kutetea Haki za Binadamu HRW limesema Kansela wa Ujerumani Angela Merkel analazimika kuzungumzia masuala ya haki za binadamanu atakapokutana na Rais wa Urusi Vladimir Putin Agosti 18.

https://p.dw.com/p/33KDf
Deutschland Merkel und Putin in Dresden - Begrüßung
Picha: picture-alliance/dpa/M. Hiekel

Kansela wa Ujerumani Angela Merkel analazimika kuzungumzia masuala ya haki za binadamanu atakapokutana na Rais wa Urusi Vladimir Putin katika mji wa Meseburg, Ujerumani, Agosti 18, limesema Shirika la Kutetea Haki za Binadamu la Human Rights Watch, Ijumaa. Msemaji wa kansela huyo amesema viongozi hao wawili watajadili vita vya Syria, mgogoro wa mashariki mwa Ukraine, na sera ya nishati.

"Mkutano huo ni fursa muhimu kwa Angela Merkel kumshinikiza rais wa Urusi juu ya masula yanayohusu haki za binadamu nchini mwake na kimataifa, "amesema Hugh Williamson, mkurugenzi wa Human Rights Watch kwa Ulaya na Asia ya Kati. "Hususana kuachiliwa huru kwa wanaharakati wa haki za binadamu waliokamatwa nchini Urusi na ulinzi kwa raia katika mapigano yanayotarajiwa jimbo la Idlib, Syria, lazima yawe juu katika ajenda ya mazungumzo yao."

Urusi imekuwa ikifanya vitendo vikubwa vya ukandamizaji hivi karibuni ambavyo havikuwahi kushuhudiwa tokea enzi za utawala wa umoja wa kisovieti. Hali hiyo ilianza 2012, kufuatia maandamano ambayo hayakuwahi kutokea ya umati mkubwa wa watu, na kupamba moto zaidi 2014 wakati Urusi ilipolitwa kwa nguvu eneo la Crimea nchini Ukraine na kujihusisha kwake na mgogoro wa mashariki mwa Ukraine. Serikali ya Urusi pia imekuwa ikikandamiza uhuru wa kujieleza katika mtandao wa intaneti na imelenga wakosoaji wengi kwa makosa yanayochochewa zaidi na kisiasa na yenye kushangaza. Kukamatwa kwa Oyub Titiev, mkurugenzi wa Chechnya wa kundi kuu la kutetea haki za binadamu la Memorial, na mtengenezaji filamu kutoka Crimea Oleg Sentsov ni mfano wa ukandamizaji mbaya unaofanywa na serikali ya Urusi.

Mashambulizi ya Syria ya silaha za sumu lazima yasite

Nchini Syria, tokea mwkaa 2015, ushirika wa kijeshi kati ya Urusi na Syria umefanya mashambulizi ya kulenga raia wa kawaida bila kuchagua, ikiwa ni pamojana kutumia silaha zilizopigwa marufuku kama vile mabomu ya kutawanyika na silaha za moto.Iwapo mashambulizi yanayotegemewa kufanyawa na muungano huo wa kiijeshinwa Urusi na Syria utafanywa katika jimbo la Idlib kwa kutumia njia hizo hizo zinazokwenda kinyume na sheria, matokeo yake yatakuwa ni raia wengi kupoteza makaazi yao pamojana kupata majeraha makubwa, limesema shirika la Human Rights Watch.

Lakini Urusi imezungumza na serikali ya Syria na kuitaka kusita utumiaji wa sialha zilizopigwa marufuku, kufanya mashambulizi ya kutochagua, yale ya kulenga raia wa kawaida.

Syrien russische Langstreckenbomber Tu-22M3
Ndege za Kirusi nchini SyriaPicha: picture-alliance/Ministry of defence of the Russian Federation

Kansela Merkel lazima amsisitize Rais Putin kuahidi kuzuia utumiaji wa silaha zilopigwa marufuku na kuwalinda raia na mashambulizi yanayokwenda kinyume na sheria.

Kansela Merkel pia anatakiwa aishinikize Urusi, ambayo ni mshirika wa karibu wa Syria, kuishawishi serikali ya Syria kusita vitendo vyake vya mateso vizuizini pamoaja na kupotea kwa raia kiholela pamoja na kuifuta Sheria namba 10, iliyopitishwa hivi karibuni inayoruhusu serikali kutaifisha mali za raia, na ambayo inafanya vigumu kwa wakimbizi wa Kisyria kurudi nchini mwao.

Maafisa wa Urusi wamekuwa wakihangaika kutafuta uungwaji mkono wa kuwarudisha nyumbani wakimbizi wa Syria, na kutaja kuwa itasaidia kuijenga tena nchini hiyo iliyoharibiwa kwa vita," anasema Williamson. " kansela Merkel lazima aweke wazi kwamba Ujerumani haitounga mkono mipango ambayo itapelekea Assad na washirika wake kufaidika kwa uhalifu wao nchini Syria."

Mwandishi: Yusra Buwayhid/HRW website

Mhariri: Iddi Ssessanga

https://www.hrw.org/news/2018/08/17/germany-put-rights-agenda-putin-meeting