1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

HRW: Misaada ya Covid-19 Afrika haikuwafikia walengwa

Sylvia Mwehozi
12 Oktoba 2021

Shirika la kimataifa la kutetea haki za binadamu, Human Rights Watch, limesema katika ripoti yake kwamba janga la Covid-19 limedhihirisha hitaji la nchi za kiafrika kuimarisha ulinzi wa mifumo ya kijamii na maisha bora. 

https://p.dw.com/p/41Z5x
Weltzeit | Traffic Jam in Lagos, Nigeria
Picha: Adeyinka Yusuf/AA/picture alliance

Serikali nyingi za kiafrika zilianzisha hatua kama za utoaji wa fedha na msaada wa chakula katika kukabiliana na ongezeko la umaskini na njaa vilivyochangiwa na janga hilo, lakini familia nyingi hazikupata msaada huo. Benki ya dunia inakadiria kuwa hadi kufikia mwishoni mwa mwaka huu, mgogoro wa Covid-19 utasababisha ongezeko la takribani Waafrika milioni 29 katika umaskini mkali.

Maus Segun ambaye ni mkurugenzi katika Human Rights Watch kanda ya Afrika anasema kuwa "serikali za kiafrika zinapaswa kuwekeza haraka katika mifumo ya ulinzi wa kijamii inayohitajika ili kuhakikisha kwamba waafrika wanaweza kuvumilia athari mbaya za janga hilo kwa heshima". 

Kati ya mwezi Machi mwaka jana na Agosti mwaka huu, Human Rights Watch iliwahoji zaidi ya watu 270 katika nchi za Cameroon, Ghana, Kenya, Nigeria na Uganda juu ya athari za janga la Covid-19 na upatikanaji wa chakula na kuishi, na jitihada za serikali katika kukabiliana na janga hilo. Watafiti walizungumza na watu binafasi walioathirika, familia, wafanyakazi wa afya, maafisa wa serikali na wawakilishi wa mashirika yasiyo ya kiserikali, taasisi za kimataifa za kifedha na wafadhili.

Weltspiegel 11.05.2021 | Corona | Kenia Nairobi | Waisenschule
Wanafunzi wengi wameathirika kwasababu ya shule kufungwaPicha: Yasuyoshi Chiba/AFP/Getty Images

Nchini Kenya na Nigeria, shirika hilo limebaini watu kupoteza ajira, kipato kupungua na kuenea kwa njaa miongoni mwa watu wanaoishi katika umaskini jijini Nairobi na Lagos. Nchini Kenya, iligundulika ongezeko la ukatili dhidi ya wanawake na wasichana wakati nchi ilipozifunga shughuli na marufuku ya kutotoka nje usiku. Huko Ghana na Uganda, kulikuwa na ongezeko la ajira kwa watoto kutokana na janga la Covid-19. Nchini Cameroon watafiti waligundua ufisadi na kukosekana kwa uwazi katika matumizi ya serikali juu ya fedha zilizokusudiwa kushughulikia athari za kiafya na kiuchumi.COVID-19 imeathiri juhudi za kupambana na Malaria

Watu waliohojiwa walidai kwamba hatua za kufunga shughuli, vizuizi vya kusafiri na hatua nyinginezo zilizoanzishwa za kudhibiti kuenea kwa virusi vya corona, zinahusiana na kuanguka kwa uchumi, kupunguza upatikanaji wa chakula na vitu vingine muhimu.

Msichana mmoja mwenye umri wa miaka 14 nchini Ghana alielezea kwamba alikosa chakula cha bure shuleni baada ya shule kufungwa na hivyo ikamlazimu kufanya kazi saa tisa ili kujikimu. Serikali nyingi za kiafrika zilifikiria kufukia mashimo katika ulinzi wa kijamii wakati wa janga la Covid-19 na kuanzisha hatua za utoaji fedha na msaada wa chakula. Lakini hata hivyo, katika nchi hizo tano, programu hizo zilifikia sehemu ndogo tu ya familia zilizokuwa na uhitaji.

Nchini Kenya kwa mfano Human Right watch iliigundua kwamba maafisa na wanasiasa waliokuwa na jukumu la kuwasajili watu katika mpango wa kupokea fedha za Covid-19 hawakujali vigezo na badala yake waliwapendelea ndugu zao na marafiki.