1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

idadi Waliokufa shambulio la bunduki Urusi yapindukia 100

23 Machi 2024

Idadi ya watu waliokufa kwenye mkasa wa shambulizi la bunduki lililotokea usiku wa kuamkia leo nchini Urusi imefikia 115 wakiwemo watoto watatu huku wengine wengi wakijeruhiwa.

https://p.dw.com/p/4e3Nw
Moscow, Urusi | Kikosi cha uokoaji kikiendelea kutafuta waathirika katika jumba la starehe lililoshambuliwa kwa bunduki
Kikosi cha uokoaji kikiendelea na kuzima moto na kutafuta waathirika baada ya shambulio la bunduki UrusiPicha: Russian Emergency Ministry Press Service/AP/picture alliance

Mkasa huo umetokea kwenye mji mkuu, Moscow na inaelezwa kwamba washambuliaji waliingia kwenye jumba moja la starehe wakiwa wameficha nyuso zao na kuanza kufyetua ovyo risasi pamoja na kuvurumisha mabomu yaliosababisha kuzuka kwa moto.

Kundi linalojiita dola la Kiislamu IS limedai kuhusika na shambulio hilo baya zaidi kutokea nchini Urusi. Waziri wa afya Urusi Mikhail Murashko amesema watu wengine kadhaa wamelazwa hospitalini kufuatia mkasa huo, wakiwemo watoto huku mmoja kati ya hao yuko katika hali mahututi.

Soma pia:Watu 60 wauawa kufuatia shambulizi kwenye tamasha la muziki

Mamlaka nchini humo imesema uchunguzi wa "kigaidi" umeanza na rais Vladimir Putin amekuwa akipokea taarifa za kila wakati. 

Tayari watu 11 ikiwemo wanne wanaoshukiwa kufanya shambulizi hilo wamekamatwa.