1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Idadi ya waliokufa China yapindukia elfu 55 na msaada wa mahema wahitajika zaidi

23 Mei 2008

-

https://p.dw.com/p/E4sY

BEIJING

Maafisa katika jimbo la Sichuan nchini China wanasema kwamba idadi ya watu waliokufa kufuatia tetemeko la ardhi wiki iliyopita imepindukia watu elfu 55 huku wengine elfu 25 wakiwa bado hawajulikani waliko.Serikali ya China imetoa mwito kwa jumuiya ya kimataifa kupeleka msaada zaidi wa mahema kwa ajili ya watu zaidi ya millioni tano ambao hawana makaazi.Maafisa katika jimbo hilo lililoathirika zaidi la Sichuan wanasema zaidi ya majumba millioni tano yaliporomoka kufuatia tetemeko kwenye eneo hilo lenye wakaazi zaidi ya millioni 28.Aidha maafisa hao wanahofia kwamba majira ya mvua huenda yakasabisha mafuriko ya ghafla katika maeneo ya nyanda za chini.Waziri mkuu wa China Wen Jiabao amekutana na walionusurika kwenye mkoa wa Beichuan eneo mojawapo liliathirika vibaya zaidi katika tetemeko la ardhi.