1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Idadi ya waliokufa kutokana na Ebola DRC yafika 170

Bruce Amani
29 Oktoba 2018

Wizara ya Afya ya Congo imesema kuwa imerekodi matukio 267 ya ugonjwa wa Ebola vikiwemo vifo vya watu 170.

https://p.dw.com/p/37Jg3
Demokratische Republik Kongo | Ebola
Picha: Getty Images/J. Wessels

Mripuko wa ugonjwa wa Ebola mashariki mwa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo umesababisha vifo vya watu 170. Wizara ya Afya ya Congo imesema kuwa imerekodi matukio 267 ya ugonjwa huo vikiwemo vifo vya watu 170.

Siku ya Ijumaa, maafisa walikuwa wameweka idadi ya vifo kuwa watu 164. Katikati ya mwezi Oktoba, maafisa wa Congo walisema wanakabiliwa na wimbi la pili la mlipuko wa Ebola katika mji wa Beni, mkoa wa Kivu Kaskazini karibu na mpaka na Uganda.

Mripuko huo wa karibuni ni wa kumi nchini Congo tangu Ebola ilipogundulika nchini humo kwa mara ya kwanza mwaka wa 1976.