1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Idara za usalama Hong Kong zaonya kitisho cha ugaidi

Saleh Mwanamilongo
25 Mei 2020

Idara za usalama za Hong Kong zimesema visa vya ugaidi vinaongezeka mjini humo kufuatia maandamano ya makundi ya watetezi wa demokrasia wanaopinga muswada wa sheria kali juu ya usalama wa taifa iliopendekezwa na China.

https://p.dw.com/p/3cj4q
Proteste in Hongkong
Picha: picture-alliance/dpa/V. Yu

Wandamanaji zaidi ya 180 tayari wamekamatwa. 

Sheria hiyo itairuhusu serikali ya Hong Kong kuanzisha vituo vya idara za China bara katika mji huo zitakazowawezesha maafisa wa China kuwakamata watu kiholela wataposhiriki katika harakati zitakazozingatiwa kuwa za kutetea demokrasia.Wasiwwasi umezuka kwenye ngazi ya kidiplomasia na kibiashara,kufuatia hali inayoendelea mjini Hong Kong.

Kwenye taarifa iliotolewa jumatatu,waziri wa usalama wa HongKong, Jhon Lee amesema kwamba ugaidi umekuwa jijini humo na shughuli zinazohatarisha usalama wa taifa ,kama vile kudai uhuru wa HongKong ,zinaongezeka.

Lee alindelea kusema kwamba mnamo kipindi cha miezi kadhaa jiji la HongKong lililokuwa miongoni mwa miji salama duniani limegeuka kuwa jiji la ghasia na umwagikaji damu. Amesema sheria za kitaifa kwa ajili ya kuhakikisha usalama na ustawi wa jiji zinahitajika.

Hongkong Polizei setzt Tränengas gegen Demonstranten ein
Mmoja ya waandamanaji aliyejeruhiwa akiwa anasaidiwa na wenzake huko jijini Hong Kong.Picha: Reuters/T. Siu

Polisi imesema iliwakamata watu 180 wakati wa maandamano ya jumapili baada ya kutumia gesi ya kutoa machozi. Maandamano hayo yamezuka upya baada ya miezi kadhaa ya utulivu.

Mkuu wa polisi wa jiji la HongKong, Chris Tang alisema kwamba toka kuanza kwa maandamano hayo mwezi juni, wameorodhesha visa 14 vinavyohusisha miripuko ambayo hutumiwa katika visa vya ugaidi duniani na wamekamata silaha 5 pamoja na risasi.

Tanga amesema kwamba polisi wanaunga mkono sheria hiyo itakayosaidia kupambana na makundi hayo yanayodai uhuru wa HongKong na kurejesha usalama wa jamii.

Kurejea kwa maandamano hayo ya juma pili, kumekiuka amri ya kutotoka nje iliyowekwa katika juhudi za kupambana na ugonjwa wa Covid-19. Wandamanaji walikuwa wakiimba nyimbo za kudai uhuru wa jiji la HongKong, madai ambayo China Bara haitaki kuyasikia.

Hongkong Demonstration gegen Chinesische Regierungspläne
Waandamanaji hao wameitisha maandamano mengine siku ya JumatanoPicha: Getty Images/AFP/A. Wallace

Mandamano yanatarajiwa kuitishwa tena jumatano wakati bunge la jiji hilo likitarajiwa kusoma kwa mara ya pili muswada wa sheria inayofanya kuwa kosa la jinai kukiuka wimbo wa taifa wa China.

Jumapili ,waziri wa fedha wa HongKong aliandika kwenye mtandao wake kwamba mswada wenyewe wa sheria ya usalama hauwathiri imani ya wawekezaji bali kutouelewa mswada huo kunaathiri imani hiyo.

Marekani, Uingereza, Australia ,Canada na nchi nyingine zilielezea wasiwasi wake kuhusu sheria hiyo ambayo inaaminika kuuwa kabisa uhuru wa ndani wa HongKong, jiji ambalo ni huru kuliko miji yote nchini China na moja wapo ya vituo muhimu vya kibiashara ulimwenguni.

Waziri wa China wa mamabo ya nje,Wang Yi amehakisha kwamba sheria inayopendekezwa haitaathiri mamlaka ya utawala wa ndani wa jiji la Hong Kong na wala haitaondoa haki na uhuru wa watu wa Hong Kong au maslahi na haki za wawekezaji vitega uchumi kutoka nje.

Hisa za HongKong ziliporomoka kwa asilimia moja jummatatu baada ya kufikia kiwango cha chini kabisa ijumaa.

Soma Zaidi: Waandamanaji 100 wazingirwa katika chuo kikuu Hong Kong