1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Imam Abdul Rauf hana mpango wa kukutana na Kasisi Terry Jones

Halima Nyanza11 Septemba 2010

Mchungaji Terry Jones asafiri hadi Mjini New York kukutana na Imam Feisal Abdul Rauf.

https://p.dw.com/p/P9ef
Nchini Afghanistan wachoma moto sanamu za Kasisi Terry Jones.Picha: AP


Imam Feisal Abdul Rauf ambaye anaongoza juhudi za ujenzi wa msikiti katika eneo lililokaribu na kilipokuwa kituo cha biashara kilichoteketezwa katika shambulio la bomu la Septemba 11, mwaka 2001 nchini Marekani, amesema hana mipango yoyote ya kukutana na kasisi wa kanisa moja nchini humo ambaye ametishia kuchoma moto nakala za kitabu kitukufu cha waislamu,Koran.

Kasisi Terry Jones wa Florida pamoja na wafuasi wake, kwa siku kadhaa walipanga kuchoma moto nakala za koran, kwa kile alichodai kuadhimisha kumbukumbu ya shambulio hilo leo Jumamosi Septemba 11.

Hata hivyo kasisi huyo amekubali kuachana na mipango yake hiyo, na kutaka kukutana na Imam Rauf.

Hata hivyo Imam Feisal Abdul Raif, ambaye anaongoza ujenzi wa msikiti huo alikanusha taaraifa hizo, kwa kusema kuwa hajawahi kuwasiliana na kasisi huyo.