1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW
JamiiIndia

India: Watu wanane wamekufa kufuatia ajali ya treni

30 Oktoba 2023

Takriban watu wanane wamekufa na wengine 20 wamejeruhiwa baada ya treni mbili kugongana kusini mashariki mwa India.

https://p.dw.com/p/4YBJc
Indien, Vizianagaram | Zugunglück
Waokozi wakiwa eneo kulikotokea ajali hiyo huko Andhra Pradesh, India: 29.10.2023Picha: AP/picture alliance

Kulingana na vyombo vya habari nchini humo, ajali hiyo ilitokea jana jioni kati ya mji wa Alamanda na Kantakapalle katika jimbo la Andhra Pradesh.

Waziri Mkuu wa India Narendra Modi ameandika kwenye ukurasa wake wa mtandao wa kijamii wa X kwamba anatoa salamu za rambirambi kwa familia zilizofiwa na kuwaombea majeruhi wapone haraka, huku akisisitiza kuwa amezungumza na maafisa wa wizara inayohusika na usafiri wa treni.

Soma pia:Papa Francis asikitishwa na ajali iliyowaua zaidi ya watu 200 India

India ina mojawapo ya mitandao mikubwa zaidi ya reli duniani na imeshuhudia maafa kadhaa kwa miaka mingi. Ajali mbaya zaidi ilitokea mwaka 1981 katika jimbo la Bihar ambapo treni ilitumbukia mtoni na kuua takriban watu 800. Mwezi Juni, mgongano wa treni tatu katika Jimbo la Odisha ulisababisha vifo vya watu 300.