1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Iran na Bolivia waahidi kuimarisha uhusiano wao

2 Septemba 2008

-

https://p.dw.com/p/F90d

TEHRAN

Rais Mahmoud Ahmedinejad na mwenzake wa Bolivia Evo Morales wameahidi kuimarisha uhisiano wao wa kiasili na ushirikiano katika nishati na nyanja ngingine za biashara na kisiasa.

Rais Evo Morales ambaye yuko Iran kwa ziara ya siku mbili iliyoanza jana amesema kwamba anaunga mkono msimamo war ais wa Iran dhidi ya ubeberu wa nchi za magharibi na kutetea haki ya wairan.

Ziara ya Morales aliyeingia maradakani mwaka 2006 nchini Bolivia itamfikisha pia nchini Libya ambako anatarajiwa kuimarisha uhusino wa kidiplomasia.

Bolivia na Iran zilianzisha uhusiano mwezi septemba wakati rais Ahmedinejad alipofanya ziara rasmi nchini humo na kutia saini mapatano ya kibiashara na nishati.Uhusiano wa pande hizo mbili unazusha wasiwasi katika serikali ya mjini Washington.