1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Iran Nyuklia

Valvur, Andrus13 Novemba 2010

Iran imetoa tarehe ya mkutano wa kujadili mpango wake wa nyuklia

https://p.dw.com/p/Q7gu
Mkuu wa sera za nje wa Umoja wa Ulaya Catherine Margaret Ashton.Picha: Picture alliance/dpa

Mkuu wa sera za nje wa Umoja wa Ulaya Catherine Ashton, amepokea ombi kutoka kwa mpatanishi mkuu wa masuala ya nyuklia wa Iran, Saeed Jalili,  la kukutana mapema mwezi ujao kujadili mpango wa nyuklia wa Iran. Wiki hii,Jalili alimuandikia Ashton barua kupendekeza  kukutana mjini Istanbul.Baada ya kushauriana na mataifa sita makuu duniani, yatakayowakilishwa na  Ashton yaani,  Marekani, Urusi, China, Ufaransa, Uingereza na Ujerumani, kiongozi huyo amekubali kukutana tarehe 5 mwezi ujao wa Desemba  ikiwa utafanyika nchini Switzerland au Austria. Iwapo pande zote mbili zitakubaliana, hiyo itakuwa ni mara ya kwanza  kwa Iran kukutana kujadili mpango wake wa nyuklia baada ya zaidi ya mwaka mmoja.

Catherine Ashton Said Dschalili, Saeed Jalili Fotomontage Kombo
Catherine Ashton na mpatanishi mkuu wa masuala ya nyuklia wa Iran, Saeed Jalili.Picha: picture-alliance/dpa/DW-Fotomontage

Wapatanishi wa nchi za Magharibi wanasema hawana tatizo na Iran kumiliki kiwanda cha nyuklia kwa matumizi ya kiraia, lakini wanataka hakikisho kwamba mpango huo hautumiwi kurutubisha kwa siri madini ya Uranium hadi kiwango cha kuweza kutengeneza silaha za nyuklia.

Mwandishi Maryam Abdalla/Rtre/Afpe

Mhariri:Prema Martin