1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Iran yadai kushambuliwa kimtandao na Israel

Sudi Mnette
12 Aprili 2021

Waziri wa Mambo ya Nje wa Iran, Mohammed Javad Zarif ameyaelezea mashambulizi ya mtandaoni dhidi ya kinu kinu cha kurutubisha madini ya Urani cha  Natanz kuwa kitendo cha kigaidi na kuitupia lawama Israel. 

https://p.dw.com/p/3rrpk
Iran Atomprogramm
Picha: Iranian Presidency Office/AP Photo/picture alliance

Kinu hicho kilichopo katikati mwa Iran ambacho, pamoja na mambo mengine kinatengeneza vifaa vya urutibishaji wa madini ya urani. Kutokana na mkasa huo wa jana Jumapili, Zarif ameibuka na kuliambia bunge la Iran kwamba mahasimu wao wamewahujumu kutokana na mafanikio waliyoyapata.

Katika mkasa huo, hakuna yeyote alijeruhiwa wala tukio la kuvuja kwa mionzi. Mwanadiplomasia huyo wa ngazi ya juu kabisa wa Iran, amenukuliwa na shirika la habari la umma la nchi hiyo IRNA, akisema kwamba pamoja na mkasa huo maijibu yao ni kuendeleza mafanikio katika nyanja zote mbili yaani upande wa mazungumzo ya nyuklia na operesheni zao za ndani.

Israel imekaa kimya dhidi ya tuhuma hizo.

Iran | Außenminister Dschawad Sarif
Waziri wa Nje ya Iran, Mohammed Javad ZarifPicha: Russian Foreign Ministry Press Service/AP Photo/picture alliance

Hadi sasa Israel, haijajibu lolote kutokana na lawama hizo za uvamizi wa kimtandao za Ir, Iranan. Lakini hapo jana Jumapili, mkuu wa jeshi la Ulinzi wa Israel, Aviv Kochavi amenukuliwa akisema hakuna kificho chochote katika operesheni za kijeshi katika mashariki ya kati. Ilionekana kama anatoa majibu kwa Iran, wakati wa hafla ya kumbukumbu vifo vya askari wa Israel huko Herzlberg, mjini Jerusalem.

Aliongeza kwa kusema bila shaka hao mahasimu wao wanatazama, wanauona uwezo wao na wanaizingatia kwa umakinini mienendo yao. Israel inautazama mpango wa nyuklia wa Iran kama kitisho kibaya kwa sababu ina makombora ya masafa marefu yenye uwezo wa kufika umbali wa kilometa 2,000, kiwango ambacho kinatoa uwezo wa kushambulia mahala popopte katika ardhi ya Israel. Na endapo makombora hayo yatatengenezwa vichwa vya makombora ya kinyukilia, Israel itakuwa katika kitisho kikali zaidi.

Iran imekana kuwa na silaha kali

Lakini serikali ya Iran kwa wakati wote imeendelea kusisitiza kwamba haina vichwa vya makombora nyuklia na kwamba itatumia makombora yake tu, kwa mashambulizi ya kulipiza kisasi.

Tukio hilo la sasa la kushambuliwa kwa kinu cha nyuklia cha Iran linatokea ikiwa ni siku chache tu, tangu kuanza kwa mazungumzo ya kuufufua mpango ya nyuklia ya 2015 baada ya rais wa awamu iliyopita wa Marekani Donald Trump kuyatelekeza.

Rais wa sasa Joe Bide anataka kufufua makubaliano hayo kati ya Iran na kundi la mataifa sita yenye nguvu duniani, kwa makubaliano ya kulidhibiti taifa hilo la Kiislamu kwa masharti ya kuliondolea vikwazo vya kiuchumi.

Vyanzo: AFP/DPA