1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Iran yahimizwa kusita kurutubisha uranium

22 Novemba 2007
https://p.dw.com/p/CRy6

Mkuu wa Shirika la Nishati ya Nyuklia la Umoja wa Mataifa-IAEA,bwana Mohammed El Baradei kwa mara nyingine tena ameihimiza Iran kutekeleza matakwa ya azimio la Umoja wa Mataifa kuhusu mradi wake wa nyuklia.Akizungumza mbele ya bodi ya IAEA mjini Vienna,Austria,El-Baradei alisema,sharti mojawapo ni kusita kurutubisha madini ya uranium. Jumuiya ya kimataifa ina hofu kuwa Tehran inajariibu kutengeneza silaha za kinyuklia.Iran mara kwa mara,imesisitiza kuwa mradi wake wa nyuklia ni kwa matumizi ya amani tu.