1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Iran yapokea zana kwa matumizi ya nishati ya Nuklia

28 Desemba 2007
https://p.dw.com/p/ChY7

TEHRAN:

Urusi imetoa sehemu ya pili ya msaada wake wa zana za nishati ya Nuklia kwa Iran.

Zana hizo ni za kutumiwa katika kinu cha Nishati za Nuklia cha Iran kilichoko Busher.Iran inapanga kufungua kinu hicho ifikapo mwisho wa mwaka ujao. Iran ilipata sehemu ya kwanza ya vipuli hivyo Disemba 17 na ifikapo mwezi Febuari mwaka ujao Iran itakuwa imepokea kwa ujumla fito nane za kinuklia.

Washington inasema kuwa sasa Iran imepokea zana hizo inafaa ikomeshe mpango wake wa kurutubisha Uranium.Nchi za magharibi zinaishuku Iran kuwa inaficha mpango wake wa silaha za Nuklia huku Tehran inasema inahitaji nuklia kwa matumizi ya nishati tu.