1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Iraq yaionya Uturuki juu ya opresheni ya kijeshi dhidi ya PKK

23 Februari 2008

-

https://p.dw.com/p/DCI6

SULAIMANIYAH

Waasi wa chama wafanyikazi wa kikurdi cha PKK wametishia kufanya mashambulio ndani ya Uturuki ikiwa jeshi la nchi hiyo halitasimamisha opresheni zake kaskazini mwa Iraq.Msemaji wa kundi hilo Ahmed Danis ameonya ikiwa Uturuki itaendelea kuwashambulia wanachama wake katika eneo la Kurdistan kaskazini mwa Iraq watachukua hatua ya kushambulia miji ya Uturuki.Aidha kundi hilo linadai kuwauwa wanajeshi 22 wa Uturuki kwenye mapigano yanayoendelea.Uturuki imesema itaendelea na opresheni hiyo hadi watakapofikia lengo lao la kuwamaliza waasi wa Pkk.Opresheni hiyo ya kijeshi ya Uturuki imeshutumiwa na serikali ya Iraq,katibu mkuu wa Umoja wa mataifa Ban Ki Moon na Marekani.

Waziri wa mambo ya nje wa Iraq Hoshiyar Zebari ameonya kwamba ingawa uvamizi huo wa Ghafla ni mdogo kwenye eneo la vijijini linaweza likasabaisha hatari kubwa kwenye eneo zima la Iraq.

Waziri wa mambo ya nje wa Marekani Condoleza Rice amesema Uturuki inapasa kutambua kwamba usalama katika Iraq pia ni kwa manufaa yake ingawa haiungi mkono waasi wa PKK.

Kundi la Pkk linalopigania kujitenga kwa eneo hilo la Kurdistan kutoka kwa Uturuki linaangaliwa kama kundi la Kigaidi na serikali ya Mjini Ankara,Marekani na Umoja wa Ulaya.