1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Ireland kufuta marufuku ya utoaji mimba

Sekione Kitojo
26 Mei 2018

Ireland imepiga kura kwa wingi mkubwa kubadilisha baadhi ya sheria kali za utoaji mimba katika bara la Ulaya jana Ijumaa(25.05.2018), kwa mujibu wa uchunguzi wa maoni katika kura hiyo ya kihistoria.

https://p.dw.com/p/2yLn0
Irland Referendum
Picha: Getty Images/J. J. Mitchell

Kura  hiyo  iliyopigwa  kwa  minajili  ya  kuondoa  marufuku  iliyomokwa mujibu  wa uchunguzi wa maoni  katika kura ya maoni ya kihistoria  katika  nchi  hiyo  ambayo kimsingi ina Wakatoliki  wengi. katika  katiba  ya  kutoa  mimba  isipokuwa  tu  katika  wakati ambapo maisha  ya  mama  yamo  hatarini ilitarajiwa  kushinda  kwa wingi  wa  theluthi  mbili ya  kura.

Irland Referendum
Mpiga kura akipokea karatasi ya kupigia kura ya maoni nchini IrelandPicha: Getty Images/AFP/B. Cronin

Uchunguzi wa  maoni  uliofanywa  na  gazeti  la  Irish Times umeonesha  kwamba  asilimia  68 ya  Waireland  walipiga  kura  ya "ndio" kufanya  mabadiliko ya  nane  ya  katiba, wakati  uchunguzi wa  maoni  uliofanywa  na  kituo  cha  televisheni  ya  taifa  RTE kimeweka  idadi  ya  wanaokubali kuwa  asilimia  69.4.

Taasisi  ya  uchunguzi  wa  maoni  ya  Ipsos/MRBI iliwauliza  zaidi ya wapiga  kura  4,500  katika  maeneo 160  ya  kupigia  kura  katika kila  jimbo  la  uchaguzi  kwa  ajili  ya  gazeti  la  Irish Times, kukiwa na  uwezekano  wa  makosa  unaokaribiwa  kuwa  asilimia  1.5.

Uchunguzi  wa  RTE ulihusisha  watu 3,800  na  ukiwa  na  wastani wa  makosa  wa  asilimia  1.6.

Umeonesha  mgawanyiko  mkubwa  miongoni  mwa  makundi  ya umri , ambapo  asilimia  87.6  ya  watu  wenye  umri  kati  ya  miaka 18-24 wakipiga  kura  ya  "Ndio" wakati  watu  wenye  umri  wa miaka  65  na  kuendelea  ni kundi  pekee  lililokataa  mabadiliko, ambapo  asilimia  58.7  walipiga  kura  ya  "Hapana".

Watu  waliojitokeza  kupiga  kura  walikuwa  wengi ambapo  katika baadhi  ya  maeneo  kumeripotiwa  idadi  ya  zaidi  ya  asilimia  70, kwa  mujibu  wa  RTE.

Irland Referendum
Mwanamke akipiga picha katika bango kubwa la picha inayoashiria haki ya mwanamke kuishi mjini DublinPicha: picture-alliance/empics/N. Carson

"Inaonekana  kuwa tutaandika  historia  kesho," waziri  mkuu  Leo Varadkar , ambaye  amefanya  kampeni  ya "Ndio" , aliandika  katika ukurasa  wa  Twitter. Matokeo  rasmi  hayatarajiwi  hadi  leo Jumamosi  mchana. Kura  hiyo  imeligawa  taifa  hilo  ambalo kimsingi  lina  waumini  wengi  wa  Kikatoliki, huku  kukiwa  na  hisia kali  katika  pande  zote  zilizoshiriki  katika  mjadala  huo.

Maisha ya mama pia  ni muhimu

Utoaji  mimba  unaruhusiwa  tu  kwa  sasa  iwapo  maisha  ya  mama yamo  hatarini lakini sio  katika matukio  ya  kubakwa  ama udhalilishaji  kingono kupitia  ndugu.

Kiongozi  wa  upinzani  wa  chama  cha  Sinn Fein Mary Lou McDonald, ambaye  pia  alifanya  kampeni ya  "Ndio" , ameieleza kura  hiyo  ya  maoni  kuwa  ni "kufunga  ahadi  na  hatma kwa sisi wote" wakati  akipiga  kura  yake  mjini  Dublin.

Irland Generationswechsel an der Spitze der Partei Sinn Fein
Mary Lou McDonald wa chama cha upinzani cha Sinn FeinPicha: picture-alliance/dpa/N. Carson

Kura  hiyo  ilifuatia  miezi kadhaa  ya  mjadala  mkali  baina  ya  wale wanaofanya kampeni ya  kura  ya  "Ndio" na "Hapana" juu  ya  iwapo nchi  hiyo  ifanye  mabadiliko  yake  ya  nane  ya  katiba, ambayo inampa mama  na  mtoto  ambaye  bado  hajazaliwa  " haki sawa  ya kuishi" iwapo  itabadilishwa.

Wapiga  kura  waliulizwa  iwapo  wanataka  kuendelea  na  sheria hiyo  ama  kuibadilisha, ambapo  iwapo  itabadilishwa  kutaongezwa kipengee  kipya  katika  katiba  ambacho  kitatoa  uwezo  kwa  bunge kuhalalisha  utoaji  mimba.

Waliokuwa  wanafanya  kampeni  ya  "Ndio" wanadai  kwamba kifungu hicho cha  sheria  kiliwazuwia  madaktari  kufanya  utoaji mimba  hata  wakati  maisha  ya  mama  yalikuwa  hatarini.

Irland Referendum | Flughafen Dublin
Loughlan akiwasili katika uwanja wa ndege wa mjini Dublin kutoka London ili kupiga kura yakePicha: picture-alliance/empics/N. Carson

Zaidi  ya  watu  milioni  3.2 waliandikishwa  kupiga  kura  katika  kura hiyo  ya  maoni , ambayo  inafuatia  miito  ya  mara  kwa  mara kutoka  Umoja  wa  mataifa  kuifanyia  mabadiliko  sheria  hiyo nchini Ireland  na  kuwa  katika  mstari  mmoja  na  viwango  vya  sheria  za kimataifa  za  haki  za  binadamu.

Mwandishi: Sekione  Kitojo / dpae

Mhariri: Caro Robi