1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Islamabad. Bhutto aachiwa kutoka kuzuizini.

11 Novemba 2007
https://p.dw.com/p/CBK5

Waziri mkuu wa zamani wa Pakistan Benazir Bhutto ameadhimishwa kuachiliwa kwake kutoka kizuizi cha nyumbani kwa kujiunga na maandamano mjini Islamabad yaliyofanywa na wafanyakazi wa vyombo vya habari wakipinga kuzuiwa kupata habari. Hii ni sehemu ya amri ya hali ya hatari ambayo imetolewa na rais Pervez Musharraf wiki moja iliyopita.

Baadaye, polisi walimzuwia Bhutto kukutana na jaji mkuu Iftikhar Chaudhry.

Bibi Bhutto amesema baadaye kuwa amekuja kumjulia hali jaji mkuu wa Pakistan, ambaye yuko chini ya kizuizi nyumbani kwake. Amesema kuwa ameambiwa kuwa jaji mkuu hawezi kutoka nyumbani kwake , lakini anaruhusiwa kukutana na watu wanaomtembelea. Kwa hiyo nimekuja kumtembelea na kumwambia kuwa chama changu kinasimamia uhuru wa mahakama. Lakini kwa bahati mbaya inaonekana kuwa utawala huu umeamua kuweka uzio wa waya na vizuizi kuzuwia ziara yangu kwa jaji mkuu. Natoa wito wa kuachiliwa jaji mkuu na majaji wote wa mahakama kuu ya Pakistan na kwa jenerali Musharraf kuleta udhabiti nchini Pakistan.