1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Islamabad. Helikopta yaanguka na kuuwa wanne.

8 Oktoba 2007
https://p.dw.com/p/C7HS

Moja kati ya helikopta zilizokuwa zinamsindikiza rais jenerali Pervez Musharraf imeanguka katika eneo la Kashmir nchini Pakistan , na kuuwa watu wanne.

Rais hakuathirika katika ajali hiyo ambayo maafisa wa jeshi wanaeleza kuwa inatokana na matatizo ya kiufundi.

Musharraf alikuwa akisafiri kwenda katika eneo la Kashmir katika maadhimisho ya mwaka wa pili baada ya kutokea tetemeko kubwa la ardhi mwaka 2005 ambayo yameuwa karibu watu 80,000.

Wakati huo huo, jeshi limesema kuwa zaidi ya wanajeshi 50 wa jeshi la Pakistan hawajulikani waliko baada ya mapigano makubwa na wanamgambo wanaounga mkono kundi la Taliban katika jimbo la kaskazini la Waziristan. Mwishoni mwa juma , kiasi cha wanamgambo 60 na zaidi ya wanajeshi 20 wameuwawa katika jimbo lenye matatizo karibu na mpaka na Afghanistan.