1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Islamabad. Jeshi lauwa wapiganaji 130.

9 Oktoba 2007
https://p.dw.com/p/C7HJ

Jeshi la Pakistan linasema kuwa wanajeshi wake wamewauwa kiasi wapiganaji 130 katika siku mbili za mapigano makali karibu na mpaka na Afghanistan. Wanajeshi 45 wa serikali pia wameuwawa katika mapigano hayo katika jimbo la kaskazini la Waziristan lililoko katika mpaka na Afghanistan. Jeshi limesema kuwa wapiganaji wanaounga mkono Taliban walipata mafunzo kamili ya kijeshi na wanapata msaada kutoka Afghanistan.