1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

ISLAMABAD: Makubaliano ya biashara huru kati ya China na Pakistan

25 Novemba 2006
https://p.dw.com/p/CCpa

China na Pakistan zimetia saini makubaliano ya biashara huru.Kuambatana na makubaliano hayo, biashara kati ya nchi hizo mbili itaongoezwa kwa mara tatu kufikia hadi dola bilioni 15 katika kipindi cha miaka mitano ijayo.Makubaliano hayo yalitiwa saini wakati wa ziara ya rais wa China Hu Jintao nchini Pakistan ikiwa ziara ya kwanza kufanywa na kiongozi wa China tangu miaka kumi.