1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

ISLAMABAD: Pakistan yasema Sharif amekwepa kushtakiwa

11 Septemba 2007
https://p.dw.com/p/CBQo

Pakistan imesema waziri mkuu wa zamani wa nchi hiyo, Nawaz Sharif, aliamua kwenda uhamishoni ili kukwepa kukamatwa na kufunguliwa mashtaka.

Nawaz Sharif alisafiri kurejea Pakistan hapo jana akiwa na matumaini ya kupambana na rais Pervez Musharaf katika uchaguzi ujao baada ya kuishi uhamishoni nchini Uingereza kwa miaka saba. Lakini makamanda wa jeshi la Pakistan waliizingira ndege yake katika uwanja wa ndege wa mjini Islamabad na muda mfupi baadaye akasafirishwa kwenda Saudi Arabia.

Waziri wa habari wa Pakistan, Tariq Azim, amekanusha madai kwamba Pakistan imemfukuza waziri mkuu huyo wa zamani na kupendekeza kuwa ni Saudi Arabia itakayoamua kama Nawaz Sharif ataweza kurejea kwenye siasa katika kipindi cha miaka mitatu ijayo.