1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

ISLAMABAD: Paksitan yaadhimisha miaka 60 ya uhuru

14 Agosti 2007
https://p.dw.com/p/CBZA

Pakistan leo imeadhimisha miaka 60 ya uhuru wake kutoka kwa Uingereza. Wapakistan wamesheherekea kwa kupandisha bendera ya nchi yao, kucheza muziki na kufanya maombi katika maeneo mbalimbali ya nchi huku usalama ukiimarishwa kukabiliana na kitisho cha mashambulio ya kigaidi.

Sherehe za maadhimisho zimefanywa kukumbuka kugawanyika kwa bara hilo dogo mnamo mwaka wa 1947 katika sehemu mbili, Pakistan yenye idadi kubwa ya waislamu na India iliyo na idadi kubwa ya Wahindi.

Watu wamenyaa kimya kwa dakika moja kukumbuka maelfu ya watu waliouwawa kwenye maandamano yaliyotokea wakati huo.

Katika ujumbe wake wa siku ya uhuru rais wa Pakistan, Pervez Musharaf, amewashawishi Wapakistan wawaunge mkono wabunge wasio na msimamo mkali wa kidini kwenye uchaguzi wa bunge unaotarajiwa kufanyika baadaye mwaka huu.

Utawala wa rais Musharaf unakabiliwa na upinzani mkali kutoka kwa wanamgambo wa kiislamu.

Nchi jirani ya India itasherehekea uhuru wake hapo kesho.