1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

ISLAMABAD : Ugaidi na itikadi kali kutokomezwa Pakistan

13 Julai 2007
https://p.dw.com/p/CBjI

Rais Pervez Musharraf wa Pakistan amelihutubia taifa kwa kuahidi kutokomeza itikadi kali kufuatia kumalizika kwa umwagaji damu kuzingirwa kwa Msikiti Mwekundu mjini Islamabad wiki hii.

Amesema anataka kusema wazi kwamba itikadi kali na ugaidi bado haukun’golewa kutoka Pakistan lakini azma yao ni kutokomeza ugaidi na siasa kali kutoka kila upenu na pembe ya nchi.

Musharraf amesema kwamba ilikuwa ni siku ya huzuni na kuomboleza kwa kuchukuwa hatua ya kuuwa wananchi wake wenyewe lakini ameapa kuzuwiya misikiti na madrasa za dini kutumiwa kueneza uwanamgambo.

Serikali ya Pakistan imesema takriban watu 106 wameuwawa katika mapambano makali kati ya wanajeshi wa serikali na wanamgambo waliokuwa wamejichimbia kwenye Msikiti Mwekundu wakiwemo wanamgambo 75 na wanajeshi 11 wa serikali.