1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

ISLAMABAD: Viongozi wanne wa upinzani wakamatwa

23 Septemba 2007
https://p.dw.com/p/CBNS

Polisi nchini Pakistan wamewakamata na kuwazuia viongozi wanne wa upinzani na wakati huo huo wamevamia makaazi ya viongozi hao katika hatua ya kuzuia vurugu zaidi zinazopinga mpango rais Pervez Musharraf wa kugombea tena kiti chake.

Viongozi hao waliokamatwa wanaunga mkono muungano wa vyama vinavyotetea demokrasia nchini Pakistan ambao umeapa kuendeleza maandamano dhidi ya utawala wa kijeshi wa jenerali Pervez Musharraf anaetaka kuiongoza tena Pakistan kwa kipindi kingine cha miaka mitano kwa kutetea kiti chake kwenye uchaguzi uliopangiwa kufanyika tarehe 6 Oktoba.

Viongozi wa upinzani nchini Pakistan wamelaani hatua ya kukamatwa viongozi wenzao wanne na wamesema kuwa huo ni ukiukaji wa haki za msingi za binadamu.