1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

ISLAMABAD:Msikiti wa Lal bado umezingirwa na polisi

5 Julai 2007
https://p.dw.com/p/CBlc

Polisi wa nchini Pakistan bado wameuzingira msikiti wa Lal katika mji mkuu wa Islamabad.

Wakati huo huo polisi wamezidisha shinikizo dhidi ya wale ambao bado wamo ndani ya msikiti huo na kuwataka wajisalimishe.

Mapema leo ilisikika milio ya risasi baada ya polisi kufanikiwa kutegua vifaa vya kulipuka nje ya msikiti huo.

Lal Masjid au msikiti mwekundu umehusika na kampeni za kuitaka serikali ya Pakistan iidhinishe baadhi ya sharia za kiislamu katika katiba ya nchi hiyo.

Takriban watu 16 wameuwawa kufuatia mapambano ya siku mbili kati ya wanafunzi wenye msimasmo mkali na polisi.

Wanafunzi 50 walikubaliwa kuondoka kutoka kwenye msikiti huo leo hii baada ya kuchunguzwa na polisi.

Mmoja kati ya viongozi wa msikiti huo alikamatwa pale alipotaka kutoroka huku akiwa amevalia mavazi ya kike.