1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

ISLAMABAD:Pakistan na Iran zapinga tuzo ya utu bora kwa Salman Rushdie

20 Juni 2007
https://p.dw.com/p/CBq4

Pakistan na Iran zimewaita mabalozi wa Uingereza katika nchi zao ili kuwasilisha malalamiko juu ya hatua ya Uingereza ya kumtunuku hadhi ya utu bora mwandishi wa vitabu Salman Rushdie.

Rushdie aliandika riwaya ya The Satanic Verses yaani beti za shetani ambayo ilizusha hisia kali kwa aliyekuwa kiongozi wa Iran Ayatollah Ruholah Khomenei na kumfanya kutoa Fatwa yaani amri ya kuuwawa dhidi ya mwandishi huyo kutokana na kutenda kufuru.

Riwaya hiyo pia iliibua upinzani mkali katika nchi za kiislamu baada ya kuchapishwa mwaka 1988.Waislamu wanasema kitabu hicho kinakufuru dhidi ya mtume Mohammad na pia kinakejeli kitabu takatifu cha Kuran na historia ya dini hiyo.