1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

ISLAMABAD:Uchunguzi waendelea kuhusu mashambulio dhidi ya msafara wa Bhutto

20 Oktoba 2007
https://p.dw.com/p/C7EF

Waziri mkuu wa zamani wa Pakistan Benazir Bhutto amesema jaribio la kutaka kumuua huenda lilifanywa na mojawapo ya makundi manne ya wanamgambo likiwemo kundi la Taliban na Al Qaeda.

Serikali imenza kuchunguza orodha hiyo ya washukiwa iliyotolewa na bi Bhutto.

Aidha Bhutto ametaka pafanyike uchunguzi juu ya kuzimika kwa taa za barabarani wakati alipokuwa akifanya ziara yake katika eneo kulikofanyika mashambulio.

Hata hivyo chama cha Pakistan Peoples Part cha bibi Bhutto kimesema licha ya shambulio hilo Bhutto amepanga kuendelea kubakia Pakistan na kushiriki kwenye uchaguzi wa bunge unaokuja.

Zaidi ya watu 130 waliuwawa na wengine 250 wakajeruhiwa kufuatia mashambulio mawili yaliyolenga kumuua Bhutto mjini Karachi.