1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

ISLAMABAD:Waziri wa Ujerumani ziarani Pakistan

5 Juni 2007
https://p.dw.com/p/CBug

Waziri wa Ulinzi wa Ujerumani Franz Josef Jung amewasili katika mji wa Pakistan Islamabad kwa mazungumzo na wakuu wa nnchi hiyo.

Jung anatarajiwa kuwa na mazungumzo na Rais Pervez Musharaff pamoja na maafisa wengine juu ya kuunganisha nguvu katika mapambano dhidi ya magaidi na wanamgambo nchini Afghanistan.

Mapema akiwa mjini New Delhi India waziri huyo wa ulinzi wa Ujerumani alielezea umuhimu wa kuweka mikakati ya kuungwa mkono na wananchi wa Afghanistan.

Ujerumani na kiasi cha wanajeshi elfu tatu nchini Afghanistan, 21 kati yao tayari wamekwishapoteza maisha nchi humo toka mwaka 2002 walipopelekwa.

Wakati huo huo mtu mwenye silaha amempiga risasi na kumuua msemaji wa serikali ya kiislam ya jimbo la kaskazini magharibi nchini Pakistan.Jimbo hilo liko mpakani na Afghanistan.

Sayed Mehd Hussein alikuwa ni mkurugenzi wa maelezo wa serikali ya jimbo hilo na alipigwa risiasi wakati alipokuwa akitoka nyumbani kwake kwenda kazini.

Polisi wamesema kuwa bado sababu ya kuawa kwake haijajulikana.