1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Israel Gaza

Abdu Said Mtullya17 Juni 2010

Baraza la mawaziri latukana tena Israel kujadili kufungua mipaka ya Gaza.

https://p.dw.com/p/Nsp9
Meli ya misaada kwa Ukanda wa Gaza.Picha: AP

Jerusalem.

Mkutano  wa  baraza  la  mawaziri  la  Israel kuangalia ulegezaji  wa  nchi  hiyo  kuizingira  Gaza, jana umemalizika  bila  kupata  uamuzi. Hii   imetokea  licha  ya ripoti  za  hapo  kabla  kuwa  mawaziri  hao  walikuwa wapige  kura  kwa  pendekezo  lililotolewa  na  waziri  mkuu Benjamin  Netanyahu  na  mjumbe   kwa  ajili   ya mashariki  ya  kati  Tony  Blair. Afisa  wa  serikali amethibitisha   kuwa  mazungumzo  hayo  yamemalizika baada  ya  karibu  saa  nane,  ambapo  mawaziri  hao  15 watakutana  tena  leo  Alhamis  kwa  ajili  ya  majadiliano zaidi  juu  ya  suala  hilo. Israel  imepata  mbinyo   mkali kutoka   jumuiya  ya  kimataifa  kufuatia  uvamizi   meli  za misaada   iliyokuwa  inakwenda   Gaza  uliosababisha watu  kadha  kuuwawa   mwezi  uliopita.