1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Israel silaha chini na Hamas

23 Desemba 2007

---

https://p.dw.com/p/CfWQ

JERUSELEM:

Waziri mkuu wa Israel Ehud Olmert amekataa mazungumzo yoyote ya kusimamisha mapigano na chama cha wapalestina cha HAMAS.Alisema kwamba jeshi la Israel litaendelea kuwahujumu wafuasi wa Hamas wenye siasa kali wanaoishambulia Israel kwa makombora kutoka mwambao wa Gaza.

Olmert alidai kwamba, hakutakua na kusimamisha mapigano hadi kwanza Hamas imeridhia masharti yaliowekwa na pande 4 zinazohusika na utaratibu wa amani wa Mashariki ya kati .

Hapo kabla, taarifa kutoka Jeruselem zilisema waziri wa ulinzi wa Israel Ehud Barak, atazuru Misri kwa mazungumzo na rais Hosni Mubarak jumatano ijayo.

Pia waziri wa Israel ametangaza mpango wa Israel wa kujenga maskani 740 ya wayahudi mashariki mwa Jeruselem.Hii itazusha hasira za wapalestina wanaodai kwa kufanya hivyo Israel inaharibu juhudi za amani.