1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Israel yafanya mashambulizi "makubwa" Syria

20 Novemba 2019

Jeshi la Israel pamoja na kundi moja linaloangalia masuala ya vita wamesema Israel Jumatano imefanya mashambulizi makubwa dhidi ya  maeneo viliko vikosi vya Iran na Syria nchini Syria na kuwauwa wapiganaji 11.

https://p.dw.com/p/3TN14
Syrien Explosion in Qamishli
Picha: picture-alliance/AP Photo/Anha

Jeshi la Israel limesema ndege zake za kijeshi zimeyapigamaeneo kadhaa ya vikosi vya Iran kwa kutumia makombora ya ardhini kuelekea hewani yaliyoshambulia mabohari na kambi za wanajeshi.

Baada ya jeshi la Syria kufyatua makombora ya hewani ya kujilinda, jeshi la Israel linasema mfumo wa ulinzi wa Syria uliharibiwa pia.

Kulingana na mkuu wa shirika la uangalizi wa haki za inadamu katika maeneo ya vita lililo na makao yake Uingereza Syria Observatory for Human Rights Rami Abdel Rahman, kati ya wapiganaji kumi na moja waliouwawa saba walikuwa wapiganaji wa kigeni ingawa hakuweza kuthibitisha iwapo wote walikuwa raia wa Iran.

Kumekuwa na vita vya chini kwa chini nchini Syria kati ya Israel na Iran

Abdel Rahman amesema raia wanne wamejeruhiwa katika mashambulizi hayo.

Syrien Autobombe in al-Bab
Athari ya shambulizi lililofanywa nchini SyriaPicha: picture-alliance/Anadolu Agency/B. Kasim

Naftali Bennett ni Waziri wa Ulinzi wa Israel.

"Sheria zimebadilika. Yeyote atakayeishambulia Israel mchana, hatolala usiku. Hivyo ndivyo ilivyofanyika wiki iliyopita na wiki hii pia. Ujumbe wetu kwa viongozi wa Iran ni huu, popote mutakapoipelekea miguu ya pweza wenu tutaikata tu," alisema Bennett.

Mashambulizi hayo ya Israel yameweka wazi kile ambacho kimeonekana kuwa vita vya chini ya maji vya Israel na hasimu wake mkuu Iran. Nchi hizo mbili zimekuwa zikishambuliana sana kutokana na Israel kusema kwamba majeshi ya Iran yameikaribia sana mipaka yake.

Nchi zenye nguvu zimeingilia kati vita vya Syria

Urusi kupitia naibu waziri wake wa masuala ya nje Mikhail Bogdanov, imelaani mashambulizi hayo ya Israel ikisema kwamba ni ukiukaji wa sheria za kimataifa. Urusi ambayo ndiyo nchi inayoiunga mkono kijeshi serikali ya Syria yenye utata imefanikiwa kuwa na usuhuba na Syria na Israel katika vita vya Syria ambavyo vimedumu kwa zaidi ya mwongo mmoja sasa.

Syrien Abwehrraketen nach israelischen Luftangriffen auf Damaskus
Kombora la hewani la Syria likielekea upande wa IsraelPicha: picture-alliance/Xinhua/A. Safarjalani

Vita vya Syria vimekuwa vigumu kutatuliwa kutokana na kuhusika kwa nchi kadhaa za nje zenye nguvu huku vikosi vya Urusi, Iran na Marekani vilivyoko nchini humo vikiwa vinaunga mkono pande tofauti.

Vita vya Syria vimewauwa zaidi ya watu 370,000 kufikia sasa na kuwapelekea mamilioni wengine kuwa bila makao.