1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Israel yafanya shambulio jingine Ukanda wa Gaza

Bruce Amani
27 Oktoba 2023

Vikosi vya Israel vikisaidiwa na ndege za kivita na droni vimefanya shambulizi la pili la ardhini katika Ukanda wa Gaza na kuyapiga maeneo ya viunga vya mji huo.

https://p.dw.com/p/4Y6JP
Magari ya jeshi la Israel yakikaribia Ukanda wa Gaza
Magari ya jeshi la Israel yakikaribia Ukanda wa GazaPicha: JINI/Xinhua/picture alliance

 Hayo ni kwa mujibu wa jeshi la Israel wakati likijiandaa kufanya uvamizi kamili wa ardhini katika eneo hilo linalotawaliwa na vuguvugu la Hamas.

Idadi ya Wapalestina waliouawa imepindukia 7,000 wakati Israel ikiendeleza wimbi la mashambulizi makali ya angani kujibu uvamizi uliofanywa na Hamas kusini mwa Israel mnamo Oktoba 7.

Soma pia:Jeshi la israel linaendelea kuushambulia Ukanda Gaza uliozingirwa huku likijiandaa na uvamizi kamili wa ardhi kwa lengo la kuiangamiza Hamas

Idadi hiyo inajumuisha zaidi ya watoto 2,900 na zaidi ya wanawake 1,500. Wakati wasiwasi ukitanda kuhusu hatima ya Wapalestina milioni 2.4 walionasa katika mashambulizi hayo ya mfululizo, viongozi wa Umoja wa Ulaya wametoa wito wa kupelekwa msaada wa dharura bila vizuwizi kupitia mbinu zozote zile ikiwemo kutengwa kwa maeneo salama ya kiutu na kusitishwa mapigano kwa muda.