1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Israel yaidhinisha ujenzi wa nyumba mpya kwa walowezi wa Kiyahudi

8 Machi 2010

<p>Israel imetoa ruhusa ya kujenga nyumba mpya za walowezi wa Kiyahudi katika Ukingo wa Magharibi, ingawa Novemba iliyopita ilitangaza kuwa ujenzi huo utasitishwa kwa muda.

https://p.dw.com/p/MNSJ
Palestinian workers walk next to a building at a construction site in the West Bank Jewish settlement of Maaleh Adumim, near Jerusalem, Monday, June 22, 2009. Israeli Prime Minister Benjamin Netanyahu, in defying U.S. pressure to freeze construction in West Bank settlements, says new homes must go up to accommodate settlers' growing families. But some 40 percent of the population growth in settlements came from people who moved there and not from growing families, according to the government's latest statistics. In the meantime, more than 5,000 new apartments have been completed over the past three years, Central Bureau of Statistics figures show. (AP Photo/Dan Balilty)
Makaazi ya walowezi wa Kiyahudi yakijengwa katika Ukingo wa Magharibi .Picha: AP

Upanuzi wa makaazi hayo ya Wayahudi katika maeneo yanayokaliwa na Israel katika Ukingo wa Magharibi, umetangazwa muda mfupi kabla ya Makamu wa Rais wa Marekani Joe Biden kuwasili nchini Israel na ni siku moja baada ya Wapalestina kukubali mazungumzo yasio moja kwa moja kufanywa pamoja na Israel.

Kuendelea kupanua makaazi ya walowezi wa Kiyahudi ni kikwazo kikubwa kabisa katika jitahada za kufufua majadiliano ya amani ya Mashariki ya Kati pamoja na Wapalestina. Licha ya jitahada za kidiplomasia zinazoongozwa na Marekani, majadiliano hayo yameahirishwa tangu miezi kumi na tano iliyopita. Wapalestina wanashikilia kuwa watarejea kwa majadiliano ya uso kwa uso,ikiwa tu Israel itakubali kusitisha kabisa ujenzi wa makaazi ya Wayahudi katika Ukingo wa Magharibi unaokaliwa na vile vile Jerusalem ya Mashariki iliyotekwa. Mwanzoni Marekani iliunga mkono dai hilo, lakini sasa inatoa mwito kwa pande zote mbili kurejea moja kwa moja katika meza ya majadiliano, huku ikiikosoa Israel mara kwa mara kwa harakati za ujenzi kama ilivyokuwa ikifanya tangu muda mrefu.

Wapalestina wamelaani tangazo hili jipya la Israel na wametoa mwito kwa Marekani kuingilia kati ili kusitisha ujenzi wa makaazi mapya. Msemaji wa Utawala wa Wapalestina, Nabil Abu Rudeina alipozungumza na shirika la habari la AFP alisema,"Israel inaendelea kuvuruga jitahada za amani. Serikali ya Marekani lazima ichukue hatua kusitisha harakati zote za ujenzi katika Ukingo wa Magharibi na Jerusalem ya Mashariki.  Hata kundi la Kiisraeli "Peace Now" linalopinga ujenzi wa makaazi hayo, limelaani ujenzi huo mpya na limesema, mpango huo utasababisha mwanya mkubwa zaidi kati ya Waisraeli na Wapalestinana.Vile vile utahatarisha suluhisho la mataifa mawili.

President Barack Obama and Vice President Joe Biden walk back to the White House, from the Blair House in Washington, Thursday, Thursday, Feb. 25, 2010, after meeting all day with Republican and Democrat lawmakers to renew his struggle to reform health care. (AP Photo/J. Scott Applewhite)
Rais Barack Obama(kushoto) na Makamu wa Rais,Joe Biden wa Marekani.Picha: AP

Makamu wa Rais wa Marekani Joe Biden anaeanza ziara yake ya siku tatu nchini Israel leo hii, amesisitiza umuhimu wa kurejea katika majadiliano ya amani. Amesema hiyo ni kwa maslahi ya Israel, Wapalestina na Marekani. Hiyo kesho Biden atakutana na Rais wa Israel Shimon Peres,Waziri Mkuu Benjamin Netanyahu na kiongozi wa upinzani  Tzipi Livni. Siku ya Jumatano, atakuwa na majadiliano pamoja na Tony Blair alie mjumbe maalum wa kundi la pande nne linalotafuta suluhisho la amani kwa mzozo wa Mashariki ya Kati. Vile vile amepanga kukutana na Rais wa Wapalestina Mahmoud Abbas na Waziri Mkuu Salam Fayyad atakapotembelea miji ya Ramallah na Bethlehem iliyo katika Ukingo wa Magharibi. Siku ya Alkhamisi Biden ataelekea Amman nchini Jordan. 

Muandishi: Martin,Prema/DPAE/AFPE

Mhariri: Othman,Miraji