1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW
SiasaIsrael

Israel yakomboa maeneo ya mpaka na Gaza

Josephat Charo
10 Oktoba 2023

Israel imesema imeyakomboa maeneo ya mpaka na Gaza kutoka kwa wanamgambo wa Hamas.

https://p.dw.com/p/4XMh7
Waziri Mkuu wa Israel Benjamin Netanyahu ametahadharisha kwamba mashambulizi ya angani ya sasa dhidi ya Gaza ni mwanzo tu, kufuatia shambulizi lao la kushtukiza dhidi ya Israel siku ya Jumamosi.
Waziri Mkuu wa Israel Benjamin Netanyahu ametahadharisha kwamba mashambulizi ya angani ya sasa dhidi ya Gaza ni mwanzo tu, kufuatia shambulizi lao la kushtukiza dhidi ya Israel siku ya Jumamosi.Picha: Lisi Niesner/REUTERS

Hayo yanajiri huku idadi ya vifo ikivuka 3,000 Jumanne, siku ya nne ya mapigano makali tangu wanamgambo hao walipofanya shambulizi la kushtukiza.

Waziri Mkuu wa Israel Benjamin Netanyahu ametahadharisha kwamba harakati ya jeshi la nchi hiyo kufuatia shambulizi la Jumamosi iliyopita ni mwanzo wa vita virefu vya kuiangamiza Hamas na kulibadili eneo la Mashariki ya Kati.

Wakati haya yakiarifiwa rais wa Ufaransa Emmanuel Maron amelaani hatua ya Hamas kutishia kuwanyonga baadhi ya mateka wapatao150 walio mikoni mwao, akisema ni vitisho visivyokubalika.

Akizungumza kwenye mkutano na waandishi habari mjini Hamburg akiwa na mwenyeji wake kansela wa Ujerumani Olaf Scholz, Macron amesema anazingatia uwezekano kwamba Hamas ilipata msaada kutoka nje kuishambulia Israel lakini akasisitiza hakuna ushahidi wowote wa kuhusika moja kwa moja kwa Iran.