1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW
MigogoroIsrael

Israel yashambulia maeneo 250 ya Ukanda wa Gaza kwa siku

John Juma
13 Desemba 2023

Jeshi la Israel limesema mapema leo kwamba vikosi vyake vimeyashambulia zaidi ya maeneo 250 katika Ukanda wa Gaza ndani ya siku moja.

https://p.dw.com/p/4a7Li
Ukanda wa Gaza | Wapalestina wakikimbia mashambulizi ya Israel
Wapalestina wakikimbia mashambulizi ya Israel kutoka mji wa kusini mwa Ukanda wa Gaza wa Khan Younis. Picha: Abed Rahim Khatib/Anadolu/picture alliance

Limeongeza kuwa vikosi vyake vilifanya mashambulizi ya umakini kutoka angani, baharini na ardhini dhidi ya ngome za "magaidi" jana Jumanne.

Kulingana na Israel, wanamgambo wa Kipalestina pia walirusha makombora kuelekea Israel leo Jumatano katika miji ya mpakani karibu na Ukanda wa Gaza.

Jeshi la Israel pia lilitangaza vifo vya wanajeshi wake 10 waliouawa Jumanne. Jumla ya wanajeshi 115 wa Israel wameuawa tangu ilipoanzisha operesheni yake ya ardhini dhidi ya Hamas, kundi ambalo Marekani, Umoja wa Ulaya na nchi nyingine hulichukulia kuwa la kigaidi.

Kulingana na wizara ya Afya ya Gaza inayodhibitiwa na Hamas, idadi ya Wapalestina waliouawa tangu vita hivyo vilipoanza Oktoba 7, imepita 18,400.