1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

ISTANBUL:Erdogan kuliomba bunge kuidhinisha hatua ya kijeshi dhidi ya waasi wa Kikurdi

11 Oktoba 2007
https://p.dw.com/p/C7Gl

Waziri mkuu wa Uturuki Recep Tayyip Erdogan anatarajiwa leo kuliomba bunge la nchi hiyo liidhinishe kuchukuliwa hatua za kijeshi dhidi ya waasi wa Kikurdi huko kaskazini mwa Irak.

Uturuki inaamini kwamba waasi hao wamekuwa wakijificha kwenye eneo hilo.

Marekani imeitahadharisha Uturuki dhidi ya kutuma vikosi vyake vya kijeshi huko kaskazini mwa Irak kuwaandama waasi hao wafuasi wa chama cha wafanyakazi wa Kikurdi cha PKK.

Msemaji wa wizara ya mambo ya nje wa Marekani Sean McCormack amesema, kwa matazamo wa nchi yake hatua ya kijeshi ya Uturuki hadi ndani ya Irak haitaleta suluhisho la kudumu.

Wanajeshi 15 wa Uturuki wameuwawa katika mashambulio ya chama cha PKK.