1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

J3 0809 News

8 Septemba 2007
https://p.dw.com/p/CBRj

Lisbon. Mawaziri wa mambo ya kigeni wa umoja wa Ulaya wazungumzia kupata msimamo wa pamoja.

Mawaziri wa mambo ya kigeni kutoka mataifa 27 wanachama wa umoja wa Ulaya wanafanya mazungumzo karibu na mji wa Porto nchini Ureno yenye lengo la kufikia msimamo wa pamoja kuhusu jimbo la Serbia la Kosovo.

Baadhi, lakini sio mataifa yote ya umoja wa Ulaya yanaunga mkono pendekezo la umoja wa mataifa ambalo litaipatia uhuru jimbo la Kosovo ambalo linakaliwa na watu wengi wenye asili ya Albania.

Serbia imesema kuwa haitaliachia kwa hiari yake jimbo hilo.

Waziri wa mambo ya kigeni wa Ujerumani Frank-Walter Steinmeir amesema kuwa majadiliano hayo yanakwenda vizuri licha ya vikwazo kadha.

Huenda nafasi sio kubwa sana, lakini nafasi ndogo ipo , lazima nikubali. Tunajaribu pamoja na wawakilishi wa kutoka Kosovo na Serbia kuikuza nafasi hii ili kuweza kupata mafanikio, amesema Steinmeier.

Umoja wa Ulaya, Russia na Marekani zinaongoza duru kadha za majadiliano baina ya pande hizo mbili yenye lengo la kufikia muafaka ifikapo mwishoni mwa mwaka huu.