1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

J3 0809 News

8 Septemba 2007
https://p.dw.com/p/CBRm

Berlin. Mtuhumiwa ataja aliyemuua Schleyer.

Karibu miaka 30 baada ya kuuwawa kwa rais wa shirikisho la waajiri nchini Ujerumani , mmoja kati ya watu wanaosadikiwa kuwa wanahusika amemtaja mtuhumiwa wa mauaji hayo.

Mwanachama wa zamani wa kundi la kikosi cha kigaidi kilichokuwa kinajulikana kama Red Army Jürgen Broock ameiambia televisheni ya taifa nchini Ujerumani kuwa Rudolf Heissler na Stefan Wisniewski alimpiga risasi Hans-Martin Schleyer na kumuua Oktoba mwaka 1977.

Broock amesema kuwa yeye pamoja na gaidi mwingine wa mwanamke kutoka kundi la RAF Brigitte Mohnhaupt waliamuru mauaji hayo.

Waendesha mashtaka wa Ujerumani wanachunguza taarifa hizo za Broock. Mapema mwaka huu uchunguzi kuhusu kuhusika kwa Wisniewski kuhusiana na mauaji hayo ulianzishwa upya. Heissler aliachiliwa huru mwaka 2001 baada ya kutumikia kifungo cha miaka 18 jela.