1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Pressefreiheit Kriegsgebiete

Kitojo, Sekione26 Mei 2008
https://p.dw.com/p/E6Ox
Eneo la Postdamer Platz mjini Berlin ambapo kutakuwa na mkutano wa baraza la vyombo vya habari duniani kuzungumzia suala la uhuru wa vyombo vya habari, kuanzia tarehe 2-4 Juni.Picha: picture-alliance/ dpa



Waandishi  wa  habari   ambao  wanaandika  habari zao  katika  maeneo  ya  vita  na  ya  hatari  huuwawa kila  mara. Kwa  hakika  wanalindwa  na  sheria, lakini kivitendo ,  sio  hivyo  kama   inavyoeleza  taasisi isiyo  ya  kiserikali  ya   waandishi  wasio  na  mipaka tawi  la  Ujerumani. Asasi   inayotetea   uhuru  wa kutoa  maoni  duniani , imewaalika   waandishi pamoja  na  wanaharakati  wa  kupigania  haki  za binadamu  mjini  Berlin , kulijadili  suala  kuhusiana na  njia  ya  kupata  utatuzi   na  sababu  zinazoleta hali  ya   kuongezeka   kwa  hatari  dhidi  ya waandishi  katika  maeneo  ya  mizozo.



Wakati  waandishi  wa  habari  wanapotoa  taarifa zao  kutoka  katika  maeneo  ya  mizozo,  taarifa  hizo zinaonyesha  hali  halisi  ya  maeneo  hayo. Kwa kufanya   hiyo  waandishi  wanapojaribu  kwa  kadiri ya  uwezo  wao  kueleza  kwa  undani,  kufanya tathmini  ya  kina   na  ikiwezekana  kuonyesha ukweli  halisi, hawahitaji  tu  kuheshimiwa  na kuthaminiwa. Ni  lazima  pia  kupata  ulinzi  kutoka katika  mataifa  hayo  yenye  mizozo, anaelezea Günter Nooke,  mjumbe wa  serikali  ya  Ujerumani akihusika  na  masuala  ya  siasa  za  haki  za binadamu na  misaada  ya  kiutu  katika  wizara  ya mambo  ya  kigeni.

Sio  tu  kwamba  mataifa  yanawajibu  wa   kulinda uhuru  wa  kutoa  maoni, na   haki  za  binadamu katika  maeneo  ya  mizozo. Baada  ya  mizozo   na kupata  amani,  na  katika  maeneo  ambayo  hayako katika  lengo   la  juu  la  kisiasa,  ni  lazima   serikali zionyeshe  umuhimu  wa  juu  katika  utoaji  habari huru  na  wa  haki  kuhusiana  na  vita  na  mizozo. Aina  hii  ya  utoaji  habari  inaleta  utatuzi  wa haraka  wa  mizozo  kutokana  na  kujua  chanzo cha  mizozo.


Mataifa  pamoja  na  serikali  mbali  mbali  zinazidi kuwaona  waandishi  wa  habari  ambao  wanapaswa kuonekana    kuwa  wanachukua  mtazamo  wa  kati katika  maeneo  yenye  migogoro, kuwa wanawaharibia. Sio  tu  utaratibu  wa  kile kinachojulikana  kama  waandishi  wanaoambatana na   wanajeshi, lakini  pia  waandishi, ambao wanajiambatisha  na  kundi  mojawapo  katika  mzozo fulani, wanajikuta  katika  hali  isiyokuwa  salama , kwa  mfano  maripota  katika  eneo  la  vita  nchini Iraq.

Hali  iko hivi  siku  hizi, wakati  kunatolewa  taarifa rasmi  na  inatangazwa  moja  kwa  moja, inawezekana  ikazimwa, na  taarifa  hiyo ikafanywa na  kundi  pinzani kuwa  ni  ya  kutatanisha. Hii  ina maana  kuwa  wakati  tunaangalia  vita  vya  ghuba , ama  kile  ambacho  waandishi  wamekuwa wakituletea  hapo  zamani, ni  sehemu tu  ya uongozi  wa  kivita  wa  Marekani, bila ya  kile ambacho  tumekuwa  tukikipata  hapo  kabla.


Anasema  Ulrich  Tilgner , mmoja  wa  maripota wanaofahamika  sana  nchini  Ujerumani  na  katika televisheni  yenye  sifa  ya  kutoa  taarifa  za  uwazi. Wakati  akifanyakazi  katika  eneo  la  mashariki  ya kati, ameripoti  kuwa , hata  katika  shirika  la  habari la  Ujerumani  kuna  hali  ya   udhibiti. Pamoja  na hayo  si  waandishi  wachache  ambao  walilazimika moja  kwa  moja  kuchunguzwa  na  mashirika  mbali mbali  ya  ujasusi. Anawaona  waandishi  wa  habari katika  hali  inayoongezeka  ya  hatari.

►◄