1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

JAKARTA: Makundi ya uokozi yaendelea kutafuta mabaki ya ndege iliyoanguka.

3 Januari 2007
https://p.dw.com/p/CCdj

Makundi ya uokozi ya nchi kavu, hewani na pia baharini nchini Indonesia yamerejea katika shughuli ya kuitafuta ndege iliyoanguka siku ya Jumatatu kutokana na hali mbaya ya hewa.

Maafisa wa serikali wameomba radhi kwa sababu ya taarifa zisizo sahihi zilizotolewa jana zikisema mabaki ya ndege hiyo yalikuwa yamepatikana na kwamba watu kumi na wawili walikuwa wamenusurika.

Ndege hiyo ilikuwa imebeba abiria mia moja na wawili.

Rubani wa ndege hiyo alikuwa amewasilisha ujumbe wa kutaka msaada wa dharura kiasi saa moja baada ya ndege hiyo kuanza safari yake kutoka kisiwa cha Java.

Ajali hiyo ya ndege ni ajali ya pili katika sekta ya uchukuzi kuikumba Indonesia katika kipindi kisichozidi juma moja.

Ijumaa iliyopita feri ilizama baharini na kusababisha maafa ya mamia ya watu.

Kufikia sasa waokoaji wamefanikiwa kuwaokoa watu mia mbili ilhali watu mia nne hawajulikani waliko.