1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Jamhuri ya Kodemokrasia ya Kongo yafuta vitambulisho vya kupigia kura

Josephat Nyiro Charo19 Julai 2010

Uchaguzi unatarajiwa kufanyika mwaka ujao ikiwa sasa imesalia miezi kumi

https://p.dw.com/p/OPPu

Wizara ya mambo ya ndani ya Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo, imefuta vitambulisho vyote vya zamani vya kupigia kura na kuwataka wapiga kura wajisajili upya kabla ya uchaguzi wa mwakani, katika kile inachoelezea kuwa ni kutaka kusawazisha daftari la wapigakura kura nchini humo.

Tayari upinzani umelalamikia hatua hiyo, ambayo huenda ikaahirisha uchaguzi, ambapo mwaka jana tume huru ya uchaguzi nchini Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo, ilianzisha operesheni ya kusahihisha daftari la wapiga kura mjini Kinshasa,licha ya operesheni hiyo kupingwa na wengi kutokana na kasoro za kiufundi.

Taarifa kamili na mwandishi wetu saleh Mwanamilongo

Mwandishi; Saleh Mwanamilongo

Mpitiaji; Thelma Mwadzaya