1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

JARKATA:Kiongozi wa tawi la Jemaa Islamiya akamatwa

13 Juni 2007
https://p.dw.com/p/CBs8

Polisi ya Indonesia imesema imemkamata Abu Dujana kiongozi wa wapiganaji wa tawi la kundi la Jemaa Islamiah.

Kundi hilo linalaumiwa kwa mashambulio ya kigaidi yaliyotokea mwaka 2002 katika eneo la Bali pamoja na hujuma nyingine kama vile mashambulio ya mwaka 2004 dhidi ya ubalozio wa Australia mjini Jarkata.

Polisi inasema imefanya uchunguzi wa DNA na kuhakikisha kwamba mtu aliyekamatwa ni Abu Dujana ambaye alikuwa akitumia majina zaidi ya sita.

Dujana alipigwa risasi ya mguu na kujeruhiwa wakati wa uvamizi uliofanywa na polisi katika eneo la Java mwishoni mwa wiki iliyopita ambapo watu wengine saba pia walikamatwa.

Watu 220 waliuwawa kwenye shambulio la bomu lililodaiwa kufanywa na kundi hilo la Jemaa Islamiah.