1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Vipi vita vya Syria vilivyooanishwa na vya Israel na Hamas

Sylvia Mwehozi
2 Novemba 2023

Vita vya wenyewe kwa wenyewe Syria viko kwenye mkwamo, lakini Je, dikteta wa Syria na mshirika wake wa Urusi wanaweza kutumia mgogoro wa Gaza kama kificho cha kufanya uhalifu wa kivita?

https://p.dw.com/p/4YKP5
Syrien I Rauch über Qamishli
Moshi ukionekana katika mji unaokaliwa na wakurdi wa Qamishil, Kaskazini Mashariki mwa SyriaPicha: Orhan Qereman/REUTERS

Mnamo Oktoba 24, mashambulizi ya angani ya ndege za Urusi yaliharibu kambi ndogo ya wakimbizi ya mahema karibu na mji  kaskazini-magharibi mwa Syria. Raia watano waliuawa kwa pamoja. Enadi Aliwi ni manusura wa Syria wa mashambulizi hayo ya Urusi. Aliieleza DW kwamba aliwapoteza ndugu zake, akiwemo mama, dada na mpwa wake. "Nilikuta kila kitu kimeharibiwa”.

Aliwi na familia yake, walioyakimbia makazi yao mara mbili wakati wa vita vya wenyewe kwa wenyewe vilivyodumu kwa muda mrefu nchini Syria, wamekuwa wakiishi hapa kwa miaka saba iliyopita.

Watu 10 wajeruhiwa katika mashambulizi kusini mwa Syria

Anaendelea kusema kwamba "mashambulizi ya Urusi yalilenga moja kwa moja mahema". Shambulio hilo la anga sio pekee kuwalenga raia katika maeneo ya kaskazini mwa Syria yanayodhibitiwa na wale wanaopinga utawala wa dikteta wa Syria Bashar Assad hivi karibuni.

Katika nusu ya kwanza ya mwezi Oktoba, shirika la kofia nyeupe la Syria, lilithibitisha kutokea mashambulizi 194 kaskazini magharibi mwa Syria. Kufikia sasa, watu 62 wameuawa na raia 230 wamejeruhiwa, lilisema shirika hilo na karibu watu 67,000 wameyahama makazi yao tena.

Uhasama wadaiwa kuongezeka tangu mwaka 2019

Mwanajeshi wa Syria akipeperusha bendera ya kuonyesha jeshi limeudhibiti mji wa Idlib
Mwanajeshi wa Syria akipeperusha bendera ya kuonyesha jeshi limeudhibiti mji wa IdlibPicha: Ammar Safarjalani/Xinhua/IMAGO

Naibu mratibu wa misaada ya kibinadamu wa Umoja wa Mataifa nchini Syria David Carden aliwatembelea raia katika mji wa Idlib ambao waliathiriwa na bomu mapema mwezi Oktoba na kueleza kwamba kumekuwa na ongezeko kubwa zaidi la uhasama tangu 2019. Wanaharakati wa Syria pia wanasema Urusi na Syria zimekuwa zikitumia tena silaha zilizopigwa marufuku chini ya sheria ya kimataifa, ikiwa ni pamoja na silaha za moto na mabomu ya kutawanyika.

Ongezeko la sasa la ghasia nchini Syria linaonekana kuanza tangu Oktoba 5, kwa shambulio dhidi ya mahafali katika chuo cha kijeshi kilichoko wilaya za kati za mji wa Homs, ambao bado unadhibitiwa na serikali ya Assad. Ndege zisizo na rubani zilizokuwa na vilipuzi zilishambulia familia zilizokuwa zimekusanyika kwa ajili ya sherehe hiyo. Watu 120 waliuawa, na wengine wengi kujeruhiwa. Serikali ya Syria ilijibu kwa kuongeza mashambulizi ya angani katika maeneo yanayoshikiliwa na upinzani kaskazini magharibi.

Hamas yafufua uhusiano na Syria, mshirika wa adui wa Israel Iran

Wakati huo huo jeshi la Uturuki pia limekuwa likishambulia kwa mabomu maeneo yanayoshikiliwa na upinzani kaskazini mashariki mwa Syria. Wiki hii, Shirika la Kutetea Haki za Binadamu la Human Rights Watch lilieleza kwamba shambulio la Uturuki lilikuwa mahsusi katika kujibu "shambulio la Oktoba 2 la kujitoa mhanga kwenye lango la wizara ya mambo ya ndani katika mji mkuu wa Uturuki, Ankara, na kuwajeruhi polisi wawili."

Serikali ya Syria yalaani mashambulizi dhidi ya Gaza

Rasi wa Syria Bashar Al Assad
Rasi wa Syria Bashar Al Assad Picha: SANA/dpa/picture alliance

Kwa maana hiyo ni kwamba mashambulizi ya anga ya Urusi na Syria pamoja na yale Uturuki yalianza kutokana na matukio kabla ya shambulio la wanamgambo wa Hamas dhidi ya Israel na kulipiza kisasi kwa Israel huko Gaza. Lakini hiyo haimaanishi kwamba wimbi la sasa la ghasia nchini Syria halihusiani kabisa na kile kinachoendelea Gaza.

Israel yazidi kusogea katika maeneo ya Gaza

Serikali ya Syria kama ilivyo kwa viongozi wengine wa mataifa ya Kiarabu, imelaani mashambulizi yanayoendelea ya Israel huko Gaza. Lakini kwa mujibu wa mkurugenzi wa progarmu ya masuala ya Afrika Mashariki na Kaskazini katika baraza la Ulaya linalohusika na mambo ya kigeni Julien Barnes-Dacey, ni kwamba Syria inaweza kuitumia nafasi hiyo kujitanabaisha kwamba inapambana na ugaidi kama inavyofanya Israel.

Watu wapatao milioni 4.5 wanaoishi katika maeneo yanayodhibitiwa na upinzani kaskazini mwa Syria wanategemea misaada ya kibinadamu, huku wengi wakiishi katika makambi.