1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Jerusalem. Gaza yatangazwa kuwa eneo la adui na Israel.

19 Septemba 2007
https://p.dw.com/p/CBON

Baraza la mawaziri nchini Israel linalokutana kujadilia masuala ya usalama wa nchi hiyo limeamua kuutangaza ukanda wa Gaza kuwa eneo la adui , kutokana na mashambulizi ya makombora kutoka kwa wapiganaji wa Kipalestina. Tangazo hilo linaweza kuleta hatua ya kusitishwa kwa mahitaji kama mafuta na mahitaji mengine katika eneo hilo wakati Israel haitalazimika na sheria ya kimataifa ya kuitaka kulipatia eneo hilo mahitaji muhimu. Chama chenye msimamo mkali cha Hamas kimeiita hatua hiyo kuwa ni ya kivita. Majeshi ya Hamas yalichukua udhibiti wa eneo la Gaza mwezi Juni baada ya kupambana na kundi la rais wa Palestina Mahmoud Abbas la Fatah.

Wakati huo huo , waziri wa mambo ya kigeni wa Marekani Condoleezza Rice amesema kuwa Marekani haitawatelekeza raia wasio na hatia wa Palestina katika ukanda wa Gaza baada ya Israel kulitangaza eneo hilo kuwa la adui. Condoleezza Rice amewasili nchini Israel ili kuweka msukumo katika uungwaji mkono wa mkutano unaotarajiwa kufanyika juu ya amani ya mashariki ya kati.