1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

JERUSALEM : Israel kuhamisha mamilioni ya dola kwa Abbas

24 Juni 2007
https://p.dw.com/p/CBol

Israel imekubali leo hii kuhamisha mamilioni ya dola kwa serikali ya dharura ya Rais Mahmoud Abbas wa Palestina hatua ambayo inakusudia kulibana kundi la Hamas linalodhibiti Ukanda wa Gaza.

Fedha hizo ambazo ni mapato ya kodi ya Wapalestina ambazo zimezuiliwa na Israel tokea Hamas ilipoingia madarakani katika uchaguzi wa mwaka 2006 ni sehemu ya mpango wa awali wa marupurupu ya kumuimarisha Abbas ambao Waziri Mkuu wa Israel Ehud Olmert yumkini akautangaza kwenye mkutano wa viongozi nchini Misri hapo kesho.

Afisa wa serikali ya Israel amesema baraza la mawaziri la Olmert limeidhinisha kuhamisha takriban dola milioni 350 kutoka dola milioni 700 ambazo Wapalestina wanasema zimekuwa zikizuiliwa na Israel.