1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Jerusalem. Israel yauwa wapiganaji wawili.

25 Juni 2007
https://p.dw.com/p/CBod

Shambulio la ndege za kijeshi za Israel limesababisha kuuwawa kwa mpiganaji mmoja wa kundi la Islamic Jihad na kuwajeruhi wengine watatu mjini Gaza.

Israel imesema watu hao walifyatulia makombora mawili ya Kassam na walikuwa wakijitayarisha kurusha kombora la tatu.

Shambulio hilo linakuja saa chache baada ya baraza la mawaziri la Israel kukubali kuhamisha dola milioni kadha ambazo zilizuiliwa na serikali ya nchi hiyo kwenda kwa serikali ya dharura inayoongozwa na rais wa Palestina Mahmoud Abbas.

Kuhamishwa kwa fedha hizo kuna lengo la kuimarisha utawala wa Abbas kufuatia kudhibitiwa kwa eneo la ukanda wa Gaza na wapiganaji wa chama cha Hamas. Israel ilizuwia fedha hizo za kodi ya Wapalestina inayofikia kiasi cha dola milioni 600 katika muda wa miezi 15 katika wakati serikali ya mamlaka ya Palestina ilikuwa ikiongozwa na chama cha Hamas.