1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Jerusalem. Olemrt na Abbas watayarishiwa mkutano.

7 Oktoba 2006
https://p.dw.com/p/CD57

Wasaidi wa ngazi ya juu wa waziri mkuu wa Israel Ehud Olmert na rais wa Palestina Mahmoud Abbas wamekutana hivi karibuni ili kupanga mkutano baina ya viongozi hao wawili.

Afisa mwandamizi wa serikali ya Israel ameliambia shirika la habari la AFP kuwa mkuu wa utumishi katika ofisi ya Olmert Yoram Turbowicz pamoja na mshauri mwandamizi, wamekutana na mkuu wa kundi linalofanya majadiliano upande wa Palestina Saeb Erekat pamoja na mmoja kati ya wasaidizi wakuu wa rais Abbas wiki mbili zilizopita ili kutayarisha njia kuhusu uwezekano wa kufanyika mkutano wa viongozi hao.

Hakuna tarehe hata hivyo iliyopangwa kwa ajili ya mkutano huo.

Waziri mkuu wa Israel ameeleza kuwapo tayari kwake kukutana na Abbas lakini juhudi za kutayarisha mkutano huo zilivunjika baada ya wapiganaji wa Kipalestina kumkamata mwanajeshi mmoja wa Israel karibu na ukanda wa Gaza Juni 25 mwaka huu.